KAMATA FURSA!

BUNI CHOO BORA CHA GHARAMA NAFUU

UTANGULIZI

Imezoeleka katika mila na desturi za Watanzania kwamba masuala mengi yanayohusu CHOO kutojadiliwa kwa kina na kwa uwazi. Tafiti zinaonyesha kuwa yapata watu milioni 30 hawatumii vyoo bora vyenye kukidhi vigezo na wengine milioni 5.3 hutumia vichaka kama sehemu zao za kujisetiri. Ni dhahiri kuwa 1/3 ya vifo vya watoto walioko chini ya umri wa miaka 5 vinahusishwa na hali duni ya matumizi ya vyoo na usafi wa mazingira. Hali hii hulighalimu taifa la Tanzania wastani wa shilingi bilioni 300/- kwa mwaka, fedha ambayo ingeweza kutumika katika shughuli nyingine za maendeleo kama vile kuboresha miundo mbinu ya elimu, maji, mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu na pembejeo za kilimo.

Watanzania walio wengi wanajua umuhimu wa kuwa na vyoo bora. Lakini jambo la kustajaabisha ni kwamba suala hili bado halijapewa kipaumbele cha kutosha katika jamii nyingi. Upo msemo katika jamii za Watanzania unasema kwamba "Nyumba haikamiliki pasipokuwa na choo". Msemo huu bado umebaki katika maneno zaidi kuliko matendo. Takwimu zinaonesha kuwa takribani watanzania milioni 40 wanatumia simu za kiganjani ilhali ni watu milioni 10 tu ndio wana vyoo bora vyenye kukidhi vigezo. Vile vile, inasadikiwa kuwa chini ya asilimia 10 ya Watanzania huosha mikono yao kwa sabuni mara baada ya kutoka chooni.

Ili kukabili changamoto hii, jitihada za makusudi zinahitajika katika kuongeza umuhimu na uhitaji wa vyoo bora miongoni mwa wananchi kwa kusisitiza zaidi ujenzi na matumizi sahihi ya vyoo bora, pia kuzingatia usafi wa kunawa mikono kwa sabuni baada ya kutoka chooni. Uhamasishaji wa kitaifa wa mabadiliko ya kimwenendo katika matumizi sahihi ya vyoo na usafi wa mazingira kwa sasa unaratibiwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na unalenga kudhibiti tatizo hili.

Upo umuhimu wa kuhakikisha upatikanaji wa vifaa vya kutosha na vya bei nafuu vinavyohitajika katika ujenzi na matengenezo ya vyoo bora na nafuu. Bila ya kufanya hivyo, kaya nyingi za mijini na vijijini zitaona kuwa vyoo bora ni jambo lisilotekelezeka kwa wepesi hivyo kuwalazimisha mara zote kuendelea kutumia vichaka kama sehemu mbadala za kujisaidia jambo linalopelekea kutokea kwa magonjwa ya milipuko ya mara kwa mara hasa wakati wa msimu wa mvua.

FUMBO

KAMATA FURSA, BUNI CHOO BORA CHA GHARAMA NAFUU ni fumbo linalolenga kuwahusisha vijana wa Kitanzania wabunifu na wajasiriamali watakao tumia maarifa na uwezo wao kuweza kupendekeza aina ya choo bora chenye kukidhi vigezo katika jamii nyingi nchini zile zenye kipato cha chini na cha juu. Ubunifu wa choo hiki unapaswa uzingatie zaidi mvuto, unafuu katika upatikanaji wa malighafi, ununuzi, ujenzi na matengenezo ya mara kwa mara.

Dhamira ya FUMBO hili sio tu kuwepo kwa choo bora, bali ni kujaribu kusisitiza mabadiliko ya kimtazamo katika kuhakikisha changamoto ya   matumizi duni ya vyoo bora inamalizika kabisa hasa wakati huu ambao taifa linaelekea kwenye uchumi wa viwanda. Kupitia uhamasishaji utakaofanywa na Clouds Media Group, kampeni ya FURSA inatarajiwa kuvutia vijana wa Kitanzania kuongoza mijadala itakayovunja kabisa ukimya na kuyaweka bayana masuala yote yanayohusu matumizi sahihi ya vyoo na usafi. Kupitia kibwagizo cha FURSA, vijana watakuwa tayari kuzijadili kwa kina changamoto zote zitokanazo na ukosefu na matumizi duni ya vyoo bora vyenye kukidhi haja na kuchangamkia fursa zilizopo kwenye ujenzi na matengenezo ya vyoo nchini kote.

UBUNIFU KATIKA FUMBO

Mbunifu atakayeibuka mshindi katika FUMBO hili ni yule atakayekuwa amekidhi vigezo vyote vya choo bora kama vilivyoainishwa katika miongozo ya usafi wa mazingira ya Wizara ya Afya.  Ubunifu wa aina ya choo bora utapaswa kuzingatia unafuu wa gharama, mila na desturi za Watanzania katika makundi yote ya wenye uwezo na wasio na uwezo. Muonekano wa choo kinachopendekezwa ni vema ukawa na mvuto na usilete hisia za kulibagua kundi lolote katika jamii.

TUZO

Mshindi katika ubunifu wa choo bora katika FUMBO la KAMATA FURSA, BUNI CHOO BORA CHA GHARAMA NAFUU atapatiwa ajira ya muda (kati ya miezi 6 hadi 12) ya kufanya kazi katika kampeni ya taifa ya kuhamasisha vyoo bora. Kupitia mshindi (mbunifu) wa FUMBO hili, wadau watahakikisha pendekezo lake la choo bora linafanyiwa majaribio, linaboreshwa na kuongezewa wigo wa matumizi katika kuhakikisha Choo hicho kinakuwa na manufaa kwa watu wengi zaidi.

Katika kipindi chote cha mafunzo kazini, mshindi wa FUMBO atapata fursa ya kufanya ziara ya mafunzo na kuongeza ujuzi katika nchi za Japan na Uingereza ambako atapata uzoefu zaidi kupitia makampuni makubwa duniani yaliyobobea katika ubunifu wa vyoo bora.

SIFA ZA WASHIRI

Ili uweze kushiriki katika FUMBO la KAMATA FURSA, BUNI  CHOO BORA CHA GHARAMA NAFUU yafuatayo yatazingatiwa:

MCHAKATO NA UKOMO WA KUPOKEA MAOMBI  vitazingatia  haya yafuatayo: