Card image cap
TAARIFA

Kwa mara nyingine tena kamata fursa tunakuletea habari njema kiganjani mwako. Waasisi wa kamata fursa tunaamini kuwa uchumi wa kati na maendeleo ya viwanda vitwawezekana kupitia ushiriki na jitihada za mtu mmoja mmoja. Hivyo basi kupitia mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Hoima hadi Tanga, tunakuletea fursa kiganjani mwako ili uweze kufaidika kupitia miradi mikubwa iliyoiburiwa na serikali. Kwa maelezo zaidi tembelea www.kamatafursa.co.tz/eacop

FURSA ZILIZOPO
AJIRA ZA MUDA MREFU
AJIRA ZA MUDA MFUPI
USAFIRISHAJI
MITAMBO
MALI GHAFI
VIFAA VYA UJENZI
UGAVI WA MAFUTA
HUDUMA ZA MALAZI
HUDUMA ZA VYAKULA
FURSA NYINGINEZO
TAARIFA ZA MRADI

Ramani 

Thamani ya Mradi: US$3.5 Billion

Umbali: Kilometa 1,445 kutoka Hoimahadi  Bandari ya Tanga. Kilometa 296 za bomba zitakua Uganda, 1149 zitakua Tanzania.

Card image cap

Njia ya Bomba:Bomba hili litaingia mkoa wa Kagera kutoka Nchini Uganda na kupitia katika mikoa ya Geita,Shinyanga,Tabora ,Singida,Dodoma na Manyara hadi Bandari ya Tanga. Vijiji 184 Tanzania vitapitiwa na bomba hilo.

MIKOA ANA WILAYA AMBAYO BOMBA LITAPITA
MKOA WILAYA
KAGERA Misenyi
  Bukoba Vijijini
  Muleba
  Biharamulo
GEITA Geita
  Chato
  Bukombe
  Mbogwe
SHINYANGA Kahama Mjini
TABORA Nzega
  Igunga
SINGILA Iramba
  Mkalama
  Singida Vijijini
MANYARA Kiteto
  Hanang
DODOMA Kondoa
  Chemba
TANGA Kilindi
  Handeni Mjini
  Korongwe Vijinini
  Muheza
  Tanga Mjini

GATI: Gati itajengwa nje kidogo ya Mji wa Tanga katika eneo la Chongoleani.

Taarifa za Bomba: Kusafirisha mapipa 216,000 ya mafuta ghafi kwa siku kwenye bomba la kipenyo cha sentimeta 61. Bomba litazikwa chini mita 1.2 ya ardhi

Utekelezaji:Mradi  utatekelezwa kwa ushirikiano wa Serikali za Uganda  (UNOC) na Tanzania (TPDC) na pia utahusisha kampuni za TOTAL E & P ya Ufaransa, TULLOW OIL ya Uingereza na China National Offshore Oil Corporation (CNOOC) ya China.

Ajira: Ujenzi wa Mradi huu unatarajiwa kuzalisha ajira  za moja kwa moja 10,000-15,0000 na ajira za muda mfupi zipatazo 30,000

Mradi kukamilika:2020