Card image cap

Nov 30 & Dec 1

TAARIFA

MaxMalipo ni kampuni iliyobuniwa na kumilikiwa na Watazania Wazalendo. Kampuni hii yenye kutoa huduma zake kwa kutumia mfumo wa TEHAMA, ni zao la programu ya FURSA . Huu ni mkakati unaoratibiwa na Clouds Media Group (CMG) ukiwa na lengo la kujenga hamasa na kufungua mianya ya shughuli za kiuchumi kwa jamii ya Watanzania. Kupitia mpango kabambe wa FURSA, kampuni ya MaxMalipo imeweza kujitanua na kutoa huduma hadi nje ya mipaka ya Tanzania. Nchi zinazonufaika na huduma za Max Malipo ni pamoja na Rwanda, Burundi, Kenya, Uganda, Zambia, Malawi na Ghana.

Muda, Nyenzo na Mtiririko wa Shindano
 1. 17 Disemba, 2017

  Uzinduzi rasmi wa shindano

 2. 17 Disemba, 2017 - 16 Januari, 2018

  Vikundi kuwasilisha maombi, taarifa na mipango yao kupitia jukwaa la Kamata Fursa

 3. 01 Februari, 2018

  Mchujo wa awamu ya kwanza kumalizika na kutangazwa washiriki 5

 4. 10 Februari, 2018 - 28 Februari, 2018

  Upigaji wa kura kwa jamii kwa vikundi 5 kupitia jukwaa la Kamata Fursa

 5. 07 Machi, 2018

  Washindi wawili Kutangazwa na kupewa zawadi ya Trekta

SHINDANO NA JINSI YA KUSHIRIKI

Mchakato wa kupata washindi utakuwa katika awamu kubwa mbili. Awamu ya kwanza ni mchujo wa waombaji wote. Hatua hii itahusisha kuangalia ubora na uhodari wa kuandaa mpango kazi na uimara wa kikundi ikiwa ni pamoja na uthibitisho kutoka kwenye mamlaka za serikali iliyosajili kikundi husika. Mchujo utateua vikundi washiriki 5 ambao mipango kazi yao na mawazo ya biashara yatashindanishwa katika hatua ya pili kwa mtindo wa kupigiwa kura kupitia jukwaa la Kamata Fursa, Mitandao ya Kijamii, maoni ya wasikilizaji na watazamaji wa Clouds FM na Clouds TV

Washindi watapatikana kupitia uwingi wa kura zitakazopatikana kwenye jukwaa la Kamata Fursa na zile za Clounds FM na Clouds TV. Njia hiiyenye kiwango cha juu kabisa cha uwazi itatumika kupata washindi wawili wa mwisho watakaofaidika na zawadi za Matrekta kutoka Max Malipo.

Kwa Muhtasari, kikundi kitatakiwa kufuata hatua zifuatazao kushiriki.

 1. Mwakilishi wa kikundi atatembelea www.kamatafursa.co.tz/maximalipo
 2. Mwakilishi atajaza fomu yenye taarifa za kikundi, mahali kilipo, kinajishughulisha na nini, usajili wake, mpango kazi na kutoa maelezo mafupi ya kwa nini wao wanashtahili kupata trekta.
 3. Mwakilishi ataambatanisha vielelezo husika (kwa kupakia kwenye mtandao)
 4. Mwakilishi atapokea ujumbe wa uthibitisho wa kupokelewa kwa ushiriki wao
 5. Baada ya muda uliopangwa kuisha, timu ya wataalamu watashiriki kuwachuja hadi kufikia vikundi vitano.
 6. Washiriki hawa watapigiwa kura kupitia mtandao wa www.kamatafursa.co.tz/maximalipo Mtu mmoja, kura moja.
 7. Wanaopiga na kupigiwa kura wataweza kusambaza kura zao kwenye mitandao ya Kijamii ili kuvutia watu wengi zaidi.
 8. Kura zao zitachanganywa na zile za majaji ili kupata washindi vikundi viwili ambavyo kila kikundi kitajishindia trekta.
JISAJILI HAPA