Card image cap

Nov 30 & Dec 1

FURSA YA SOKO LA MAZIWA GHAFI (RAW MILK)

Kiwanda cha TANGAFRESH kimeongeza uwezo wa uzalishaji wa maziwa kutoka lita 50,000 hadi lita 120,000 kwa siku kuanzia Januari 2018.

Hivyo kwa sasa kiwanda kinahitaji maziwa ghafi ya ziada yapatayo lita 80,000 kwa siku (awali kiwanda kilikua na uhaba wa lita 10,000 za maziwa ghafi kwa siku).

Hitaji hili la maziwa ni fursa kwa wajasiriamali na wafugaji wanaohitaji soko la uhakika la maziwa ghafi.

TAARIFA

Tangafresh inanunua maziwa ghafi kutoka kwa wazalishaji/ wafugaji na bei ni mapatano kati ya Kiwanda na Wafugaji kulingana na hali ya soko, kwenye vituo maalumu vinavyoratibiwa na Tangafresh kama inavyoonekana hapa chini.

Mkoa Mahali kituo kilipo Mratibu Mawasliano
Pwani Lugoba Shaban Mcharo 0785-465357
Mbwewe Said Salim Yoel 0712-934888
Kilimanjaro West Kilimanjaro Mary Mmary 0655-979919
Kondik Diary Processing Plant Peter Odullah 0784-583548
Morogoro Kimamba Said Salim Yoel 0712-934888
Dakawa Farm TEC Michael Mashaga 0784-739594
Dakawa Town Gudluck Luoga 0715-156320
Tanga Tanga Fresh Ltd Annadomana Nyanga 0764-230007
Tanga Fresh Ltd Samwel Sikay 0753-150769
Tanga Fresh Ltd Mussa Mpungwe 0785-202064
MAARIFA

Bidhaa za Tangafresh zinasindikwa kwa kuzingatia ubora wa hali juu kukidhi viwango vinavyohitajika Tanzania na kimataifa. Wajasiriamali na wafugaji wanatakiwa kukidhi viwango vyote vya Ubora wa maziwa ili kuweza kuuza maziwa ghafi kwenye vituo vinavyoratibiwa na Tangafresh.

Tangafresh inatoa msaada/huduma za kitaamu kwa wafugaji ili kuwawezesha kukidhi viwango tajwa hapo juu. Hii ni pamoja na (i) ushauri na mbinu ya kupata mbegu bora ya ngómbe wa maziwa (ii) ushauri na mbinu za ufugaji wa kisasa wa ngómbe wa maziwa na (iii) Kufanya utafiti na kutoa mafunzo ya ufugaji wa kisasa wa ngómbe wa maziwa kwa wafugaji


Kwa maelezo zaidi kuhusu fursa hii adimu huu wasiliana kupitia:

Mussa Mpungwe
Afisa Ukusanyaji Maziwa
Tangafresh Limited
0785-202064
0753-150769