SHUJAA WA BLUU#SHUJAA WA BLUU

SHUJAA WA BLUU NI NANI?

 

Shujaa Wa Bluu ni mtu yeyote yule atakayechukua jukumu la kuingoza jamii inayomzunguka katika harakati za kuboresha vyoo kwa kutumia bidhaa ya SATO. 

 

MAELEZO KWA MUHTASARI

 

Kampuni ya Eco Valley Advisers ambao ni wadau wa program ya Fursa na kampeni ya kitaifa ya usafi wa mazingira ijulikanayo kwa jina la #USICHUKULIE POA NYUMBA NI CHOO wameandaa shindano maalumu kuhamasisha uboreshaji na ujenzi wa vyoo bora nchini. Shidano hili linalenga kutambulisha bidhaa ya SATO ambayo ni ubunifu wa kisasa unaotoa fursa kwa wajasiriamali kujiongezea kipato sambamba na kutoa suluhisho ya kuboresha vyoo kwenye taasisi na kaya zipatazo milioni sita zenye mahitaji. Ujio wa bidhaa ya SATO utaondoa changamoto zote za kiafya zinazoanzia chooni na kufungua fursa za kipato kwa wajisiriamali watakaoshiriki kuingiza bidhaa ya SATO sokoni. 

 

FURSA YA UUZAJI WA BIDHAA YA SATO KWA WAJASIRIAMALI

 

Bidhaa ya SATO inapatikana sokoni  kwa bei ya jumla ya Shilingi 8,600/- na kuuzwa kwa bei ya rejareja ya kikomo isiyozidi shilingi 11,500/- kwa mlaji wa mwisho. Hii ni fursa adhimu, kwa maana ya kwamba mjasiriamali kadiri ya jitiahada na ubunifu wake anaweza kujipatia ziada ya shilingi 2,900/- kwa kila choo atakachouza kwa mteja wa mwisho.

 

FAIDA ZA KUSHIRIKI KWENYE SHINDANO

 

Kila mjasiriamali au mtu yeyote atakaejihusisha na uuzaji  au ununuzi wa bidhaa ya SATO atanufaika na mambo yafuatayo:

·      Muuzaji atapata faida kwa kila choo atakachouza 

·      Muuzaji atapewa ziada ya bonus ya shilingi 500/- kwa kila choo atakachouza

·      Mnunuzi atapewa bonus ya shilingi 500/- kwa kila choo atakachonunua 

·      Muuzaji na mnunuzi atapata tuzo ya heshima ya shujaa wa blue kutambua  jitihada zake za kuboresha  usafi wa mazingira

 

WALENGWA/WASHIRIKI


Shindano hili linawalenga wananchi na wajasiriamali wote nchini Tanzania, jinsia zote, vikundi vya biashara, kiuchumi, wamiliki wa maduka ya vifaa vya ujenzi, mafundi n.k. popote walipo-mijini na vijijini. 

 

JINSI YA KUSHIRIKI 


1.     Wauzaji na wasambazaji wote wa bidhaa ya SATO walio hakikiwa kushiriki kwenye shindano lazima wamesajiliwe nakupewa namba maalumu ya utambulisha. Mfano: Muuzaji Isa Hamisi hapo juu amepewa namba ya utambulisho: S0014

 

2.      Kila mnunuaji anaponunua bidhaa kutoka kwa muuzaji/msambazaji aliyesajiliwa anaweza kushiriki kwenye shindano kwa kutuma ujumbe wenye namba ya utambulisho wa muuzaji ikifuatiwa na idadi ya vyoo vya sato alivyonunua kwenda namba  0689 140 256.

Mfano:S0014 8, ikimaanisha kwamba mnunuzi amenunua vyoo 8 vya SATO kutoka kwa muuzaji Issa Hamisi mwenye namba ya utambulisho S0014

 

3.     Mnunuaji atapokea ujumbe mfupi wa kuthibitisha kupokelewa kwa taarifa yake kwenye shindano kila anunuapo bidhaa na kutuma ujumbe.

 

4.     Taarifa zote zilizopokelewa zitahakikiwa kabla ya mnunuaji kulipwa bonus yake kadiri ya vyoo atakavyokua amenunua

 

5.     Mnunuzi anaweza kutuma ujumbe kadiri awezavyo kila mara atakapo nunua bidhaa ya SATO kuendelea kujishindia bonus kadiri awezavyo muda wote wa shindano.


VIGEZO/MASHARTI

 

1.     Wauzaji wote wa bidhaa ya SATO watakaoshiri kwenye shindano hili lazima wasajiliwe rasmi. Tupigie kupitia simu +255 738 845 630

 

2.     Mnunuzi anayetaka kushiriki kwenye shindano hili lazima anunue bidhaa ya SATO kwa wauzaji/Wasambazaji waliosajiliwa na kupewa namba za utambulisho. Tarakimu nne za mwanzo lazima ziwe na utambulisho kwa mfano: S001, S0014 n.k

 

3.     Muuzaji atunze risiti au kumbukumbu za mauzo kwa uhakiki kwa muda usiopungua miezi 3 baada ya shindano kufungwa

 

4.     Mnunuzi atunze risiti au kumbukumbu za manunuzi kwa uhakiki kwa muda usiopungua miezi 3 baada ya shindano kufungwa

 

5.     Shidano hili litadumu msimu wote wa fursa 2018 kuanzia tarehe 29.9.2018

 

6.     Waandaaji wa shindano hili kampuni ya Ecovalley Advisers tunayo haki na mamlaka ya  kubadilisha au kuboresha vigezo na masharti na muongozo wa kushiri shindano hili. 

 

 


Maoni


Umesajiliwa? Ingia Haujasajiliwa? Jiunge