Taarifa Mbalimbali

Tunakuletea taarifa za fursa mbalimbali za kibiashara, uchumi na uzalishaji wa bidhaa mbali mbali

2018-09-22 12:49:52

FURSA YA UUZAJI WA VYOO BORA VYA SATO

Uuzaji wa vyoo vya SATO ni FURSA kwa wajasiriamali wote wenye uwezo na nia ya kuwa wauzaji wa vyoo vya SATO hasa wakati huu wa kampeni ya kitaifa ya usafi wa mazingira ijulikanayo kama #USICHUKULIE POA NYUMBA NI CHOO.

2018-09-22 13:17:32

FURSA ZA BIASHARA VISIWA VYA COMORO

Visiwa vya Comoro vinamahitaji makubwa ya Nyama, Mazao ya jamii ya kunde, viazi, mboga za majani na matunda. Udugu, uhusiano mzuri na ujirani wa karibu kati ya Tanzania na Comoro ni fursa kubwa kwa wajasiriamali wa kitanzania kupata masoko.

2018-09-22 13:43:32

FURSA YA SOKO LA MBEGU ZA MAFUTA YA ALIZETI

Uhitaji wa mafuta ya kula hasa mafuta ya alizeti ni mkubwa sana kwani mahitaji ni kati ya tani 400,000 hadi tani 570,000 kwa mwaka wakati soko la ndani linachangia tani 210,000 pekee na kuacha zaidi ya tani 360,000 zikiagizwa kutoka nje ya nchi kila mwaka

2018-10-17 16:39:28

MFUMO WA KUSAJILI MAFUNDI NA KUWAUNGANISHA NA WATEJA

Application ya Fundi247 ni mahususi kwa mafundi wanaotafuta fursa za ajira kwa wateja binafsi, makampuni na miradi mikubwa inayoendelea nchini. Mfumo huu ni fursa pia kwa wateja binafsi na makampuni yanayojihusisha na kandarasi mbalimbali.

Shujaa wa Bluu
Shujaa wa Bluu
Fursa Kiganjani