Taarifa Mbalimbali

Tunakuletea taarifa za fursa mbalimbali za kibiashara, uchumi na uzalishaji wa bidhaa mbali mbali

FURSA ZA BIASHARA VISIWA VYA COMORO


UTANGULIZI 

UBALOZI wa Tanzania katika Muungano wa visiwa vya Comoro unatoa wito kwa wajasiriamali wadogo na wa kati kuchangamkia FURSA za biashara zilizopo nchini Comoro. Hii ni kutokana na ukweli kwamba visiwa vya Comoro vinakabiriwa na changamoto kubwa ya uzalishaji na uhaba wa bidhaa kwa mahitaji ya ndani, hivyo kutengemea bidhaa kutoka nje ya nchi kukidhi mahitaji ya watu wapatao 800,000 visiwani humo. 

USAFIRI 

Shirika la Ndege la Air Tanzania (ATCL) linafanya safari zake kuelekea Comoro mara 3 kwa wiki: Jumanne, Alhamisi na Jumamosi. Meli ya MV Maendeleo kutoka Zanzbar inatarajia kuanza safari zake kuelekea Comoro ndani ya kipindi cha Miezi 3 ijayo kuanzia sasa.

UWEZESHAJI 

Ili kufanikisha biashara yako, ubalozi wa Tanzania nchini Comoro watakupa taarifa unazohitaji kadiri ya mahitaji ya biashara zako.

KWA MAELEZO NA TAARIFA ZAIDI WASILIANA NA: Mudrick Soragha Afisa Ubalozi wa Tanzania, Comoro Simu: +255 719 697 511 (WhatsApp) au kwa Barua Pepe: mr.soragha@gmail.com


Maoni


Umesajiliwa? Ingia Haujasajiliwa? Jiunge