Taarifa Mbalimbali

Tunakuletea taarifa za fursa mbalimbali za kibiashara, uchumi na uzalishaji wa bidhaa mbali mbali

FURSA YA SOKO LA MBEGU ZA MAFUTA YA ALIZETI


UTANGULIZI 

OBRI Tanzania ni kiwanda kinachofanya kazi na wakulima wa zao la alizeti nchini kwa kununua malighafi (mbegu za alizeti) moja kwa moja kutoka kwa wakulima wa alizeti na kisha kuongeza thamani kwa kuchakata mafuta safi ya alizeti kwa bei poa yenye kukidhi mahitaji ya walaji hasa wenye kipato kidogo. Kwa sasa Kiwanda cha OBRI kina uwezo wa kuchakata hadi lita 5,000 za mafuta kwa siku ikiwa na lengo la kuongeza uzalishaji hadi lita 15,000 kwa siku ifikapo June 2019.

FURSA 

Uhitaji mkubwa wa bidhaa hii ya mafuta ya kupikia ni fursa kubwa kwa wakulima wa mbegu za alizeti wenye kuweza kuhakikisha usambazaji wa mbegu bora za alizeti zenye kuleta tija hasa kwa viwanda vidogo vya kukamua mafuta kama OBRI ili kupunguza au kusitisha kabisa uagizaji wa mafuta ya kula kutoka nje na kuweza kukidhi mahitaji ya kila siku ya walaji.

BEI NA UTARATIBU WA MANUNUZI 

Kampuni ya OBRI inanunua malighafi (mbegu za alizeti) kutoka kwa wakulima wa alizeti moja kwa moja kwa bei ya soko na inalipa kwa wakati. Wakulima wetu wa sasa wapo wilaya za masasi,nachingwea,lindi na mtwara ambapo tunakusanya mbegu kutoka kwao na kuzichakata kisa kusambaza mafuta kwa wateja wetu maeneo mbalimbali nchini.

UWEZESHAJI 

Mafuta ya alizeti ya kupikia yenye chapa ya OBRI yanatengenezwa kwa kuzingatia vigezo vyote vya uzalishaji wa bidhaa ya kula nchini na ina vibali kutoka shirika la chakula na madawa TFDA pamoja na shirika la udhibiti wa viwango Tanzania (TBS). Zaidi ya kutengeneza bidhaa bora yenye kuzingatia kipato cha walaji nchini, kampuni ya OBRI pia inatoa mafunzo bora ya kilimo kwa wakulima wa mbegu za alizeti na namna bora ya uhifadhi wa mbegu ili kupata bidhaa bora. Vile vile tunatoa kipaumbele zaidi kwa wakulima wanawake/wakina mama ili kuweza kuwainua kiuchumi kwa kuwapa mafunzo na kuwapa soko la uhakika la mazao yao.

KWA MAELEZO NA TAARIFA ZAIDI WASILIANA NASI KUPITIA SIMU: +255 625 993 746


Maoni


Umesajiliwa? Ingia Haujasajiliwa? Jiunge