Taarifa Mbalimbali

Tunakuletea taarifa za fursa mbalimbali za kibiashara, uchumi na uzalishaji wa bidhaa mbali mbali

MFUMO WA KUSAJILI MAFUNDI NA KUWAUNGANISHA NA WATEJA


UTANGULIZI

 

WS TECHNOLOGY CONSULTING COMPANY, ni kampuni inayohusika na masuala ya teknolojia iliyopo Dar Es Salaam, Tanzania. Kwa sasa, kampuni yetu imeleta sokoni application ya Fundi247 ambayo inatumika kuwaunganisha mafundi wa aina mbalimbali na wateja Tanzania nzima. 

Kwa sasa tuna mafundi waliohakikiwa 2,300 wenye nyanja mbali mbali za ufundi kwenye mikoa zaidi ya saba ikiwemo Dar Es Salaam, Dodoma, Tanga, Morogoro, Lindi, Mtwara, Iringa na Arusha. Mafundi wetu wanatokea kwenye vyuo mbali mbali vya ufundi  kama VETA, DIT, NIT na Mgulani n.k.

 

FURSA

 

Application ya Fundi247 ni mahususi kwa mafundi wanaotafuta fursa za ajira kwa wateja binafsi, makampuni na miradi mikubwa inayoendelea nchini. Mfumo huu ni fursa pia kwa wateja binafsi na makampuni yanayojihusisha na kandarasi mbalimbali kwa vile unawawezesha kupata mafundi wenye ujuzi na waliohakikiwa.

 

UTARATIBU WA KUJISAJILI

 

Mafundi wanaojiunga kwenye mfumo wa Fundi247 wanatakiwa kua na utambulisho wa ujuzi wao katika eneo husika na  wanahakikiwa kwa kuangalia vitambulisho vyao (Mfano: kadi ya mpiga kura, leseni ya gari, au kitambulisho cha taifa) kabla hawajaingizwa rasmi kwenye mfumo wetu.

 

Application ya Fundi247 inapatikana kwa watumiaji wa simu za Android pamoja na IOS. Pia unaweza tembelea website yetu www.fundi247.com

 

MAWASILIANO

 

Kwa maelezo zaidi kuhusu mfumo wetu tupigie kupitia simu namba za simu 0683 833 630 au 0738 845 630.

  


Maoni


Umesajiliwa? Ingia Haujasajiliwa? Jiunge