Taarifa Mbalimbali

Kamata Fursa inakuletea taarifa mbalimbali za ndani na nje ya nchi.

TOTAL STARTUPPER OF THE YEAR CHALLENGE (2018-2019)


UTANGULIZI

KAMPUNI ya Mafuta ya TOTAL imeazisha shindano la  Startupper of the Year Challenge kwa ajili  wabunifu wa mawazo ya biashara na kupata  fursa ya ya mtaji pamoja na mafunzo maalumu kwaajili ya uendeshaji wa biashara hizo. 


Shindano hilo la pili kufanyika nchini linaloendeshwa na Kampuni ya Mafuta  ya TOTAL Tanzania na limewalenga vijana wenye mawazo ya biashara na miradi inayoweza kuleta mabadiliko chanya kwenye jamii zao. Mawazo ya Miradi hiyo itapimwa kulingana na wazo la ubunifu wa asili, umuhimu kwa jamii pamoja na uwezekano wa mradi kuwa endelevu.


FURSA

Washindi watatu watapata fursa ya mtaji pamoja na mafunzo maalumu kwaajili ya uendeshaji wa biashara hizo.Mshindi wa Kwanza atapata Kiasi cha Sh.Milioni 30,wa pili Sh. milioni 20 pamoja na mshindi wa tatu atapata Sh.milioni 15 kwaajili ya kuwezesha utekelezaji wa miradi watakayoibuni hapa nchini.


VIGEZO NA MASHARTI

Wabunifu watakaoshiriki wanatakiwa kuwa na biashara ya isiyozidi miaka miwili au chini pamoja na wale wenye mawazo mapya. Pia, mshiriki awe raia wa Tanzania na umri usiozidi miaka 35.


MUDA NA JINSI YA KUSHIRIKI


Shindano hili limefunguliwa Oktoba Tisa na litaisha mwezi Novemba Mwaka huu. Kushiriki na kujua utaratibu zaidi tembelea tovuti ya Total: https://startupper.total.com/en/challenges/startupper-total  


Maoni


Umesajiliwa? Ingia Haujasajiliwa? Jiunge