Fursa Taarifa

Card image cap

UWAKALA WA USAMBAZAJI WA VYOO BORA VYA BEI NAFUU VYA ‘SATO’ Oct 28, 2017

UTANGULIZI

CHOO BORA CHA SATO kimebuniwa kwa kutumia teknolojia ya kisasa ili kiweze kutumika katika vyoo vya kawaida vya shimo.
Hiki ni choo kilichobuniwa kwa ufundi na ustadi  wa hali ya juu. Sifa zake kuu ni pamoja na hizi zifuatazo:
  • Ni rahisi kukijenga kwa kwa kutumia mafundi waashi wanaopatikana maeneo yote nchini
  • Choo kinao mfuniko maalumu kwa chini wenye kujifungua na kujifunga baada ya matumizi hivyo kuweza kuzuia harufu mbaya ya chooni
  • Kuhakikisha usalama kwa watoto
  • Mfuniko unaouwezo wa kuthibiti wadudu kama mende na inzi ambao hutoka chooni na kusambaza magonjwa kupitia vyakula
WITO
Kampuni ya vyoo bora ya SATO inakaribisha maombi  kutoka kwa wajasiriamali wote wenye uwezo na niaya kuwa mawakalawa kusambaza na kuuza vyoo hivi  nchi nzima.(Taanzania)

SIFA NA VIGEZO
Mwombaji awe na mtaji usiopungua  152,000 tzs kama kianzio cha biashara yake.

USAMBAZAJI
Kampuni ya SATO itakuletea bidhaa moja kwa moja kwenye ghala au duka lako mahali uiipo

UWEZESHAJI
Ili kufanikisha biashara yako, kampuni ya SATO itakusaidia kwa kukupa vifaa vitakavyosaidia matangazo na kuvutia wateja kama vile T-shirits, mabango, vipeperushi, majarida, mafunzo ya  muda mfupi juu ya faidia na matumizi ya choo bora na mafunzo juu ya ujenzi wa choo.

BEI
Kila wakala atanunua choo kimoja kwa 7,600 tzs na kukiuza kwa 11,500 tzs

UZALISHAJI
Silafrica Tanzania limited ndiye atakayekuwa mzalishaji na msambazaji mkuu wa bidhaa za SATO nchini Tanzania.

KWA MAELEZO NA TAARIFA ZAIDI WASILIANA NA:
JUSTIN JUSTICE MBOWE
COUNTRY MANAGER
CALL:0787 312 460,0713 974922
Email:Justin.mbowe@lixil.com
Au
ALPESH PATEL
COUNTRY LEADER
SILAFRICA TANZANIA LIMITED
PUGU ROAD DAR ES SALAAM TANZANIA
CALL:0784 800 199
Email:alpesh@silafrica.com

Read more
Card image cap

Shindano la “Kamata Fursa, Buni Choo Bora Cha Gharama Nafuu” limezinduliwa rasmi Aug 31, 2017

Mchongo mpya mjini! KAMATA FURSA, BUNI CHOO BORA CHA GHARAMA NAFUU ni shindamo linalotoa Fursa kwa vijana wabunifu kubuni choo bora kwa wote, wale zenye kipato cha chini na cha juu.  

Fursa hii inawapa nafasi vijana wa Kitanzania wabunifu nawajasiriamali watakao tumia maarifa na uwezo wao kuweza kupendekezaaina ya choo bora chenye kukidhi vigezo katika maeneo ya jamii nyingi Tanzania.  

Ubunifu wa choo hikiunapaswa uzingatie zaidi mvuto, unafuu katika upatikanaji wa malighafi,ununuzi, ujezi na matengenezo ya mara kwa mara.  

Dhamira ya shindano hili sio tu kuwepo kwa choo bora, bali ni kujaribukusisitiza mabadiliko ya kimtazamo katika kuhakikisha changamoto yamatumizi yasiyokidhi ya vyoo bora inamalizika kabisa hasa taifalinapoelekea kwenye uchumi wa viwanda.  

Kupitia uhamasishaji unaofanywa na Clouds Media Group, kampeni ya FURSA inatarajiwakuvutia vijana wa Kitanzania na kuongoza mijadala itakayovunja kabisaukimya na kuyaweka bayana masuala yote yahusuyo matumizi sahihi yavyoo na usafi. Kupitia kibwagizo cha FURSA, vijana watakuwa tayarikuzijadili kwa kina changamoto zote zitokanazo na ukosefu na matumiziduni ya vyoo bora vyenye kukidhi haja na kuchangamkia fursa zilizopokwenye ujenzi na matengenezo ya vyoo nchini kote.  

Kusoma zaidi kuhusu shindano hili na kujaza fomu za ushiriki fuatilia hapa: www.kamatafursa.co.tz/challenge
 
Read more